SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 25 Mei 2017

T media news

JINSI YA KUONDOA HARUFU MBAYA MIGUUNI NA KWENYE VIATU


Tatizo la kunuka miguu na viatu linaweza kujima amani sana, hasa unapo kuwa kwenye watu na ukatakiwe uvue viatu, pia unaweza ukakera watu wengine kwa harufu, ni shida jamani. Tatizo hili wanalo sana wanaume kuliko wanawake, jamani tusome tusaidie kuelimisha wenzetu.

Mtu anapovaa viatu vya kufunika muda mrefu, labda  mtu yupo kazini asubuhi hadi jioni, ukiongeza na soksi hupelekea joto ndani ya viatu, na jasho kutoka miguuni linaingia mpaka kwenye soksi na viatu vyenyewe, na sababu hewa inakua haipiti miguuni, hapo ndipo viatu na miguu vinaanza kunuka. Pia wengine inatokana na kutofua soksi, na kutosafisha viatu mara kwa mara na kuacha fungus miguuni bila kutibia kwa muda mrefu.

Kuondoa tatizo la harufu mbaya miguuni na kwenye viatu wala sio kazi kubwa ni kuzingatia usafi wa miguu na viatu;

1.  Kila jioni mtu mwenye tatizo hili anatakiwa aoshe miguu yake na maji ya uvuguvugu vizuri kwa kutumia medicated soap kama dettol, hasa katikati ya vidole, kisha akaushe vizuri, na kuiacha ipate hewa.

2  Usirudie kuvaa soksi bila kuifua kwanza itazidisha kutoa harufu. Na hakikisha soksi unapovaliwa iwe imekauka vizuri ikiwa na ubichi itaongeza matatizo zaidi.

3. Usirudie kuvaa viatu hivyo hivyo mara kwa mara, mtu mwenye tatizo la kutoa harufu kwenye miguu na viatu, anatakiwa awe na walau pair mbili za viatu. Ili pair moja akivaa leo kesho anavaa pair nyingine huku ile nyingine anaianika mahala pakavu penye hewa ya kutosha ili kukausha unyevu nyevu ndani ya viatu, inasaidia sana kupunguza harufu.

4.  Viatu katika hali ya usafi, ili kuondoa harufu kwenye viatu ni vizuri viatu vikasafishwa vizuri na kuachwa vikauke. Viatu  vinavyoweza kufuliwa kama raba ni vizuri kufanya hivyo mara kwa mara na kuachwa juani vikauke. Viatu vingine kama vya ngozi,
- chukua baking soda au  powder  nyunyizia ndani ya viatu kisha  vianike hata kwa saa moja au zaidi, kisha vitoe vikungute na visafishe kwa ndani na kitambaa kikavu,  na viache vipate hewa, baking powder inasaidia sana kutoa harufu.
- au weka dettol ya maji kidogo kwenye pamba au maji ya ndimu , kisha safisha viatu kwa ndani, ukimaliza weka maganda ya ndimu au chungwa ndani ya viatu, au tea bags au maua ya jasmini, au maua yeyote yenye harufu nzuri kisha weka viatu sehemu yenye hewa safi na kimvuli kwa muda mrefu itasaidia kuondoa harufu mbaya.

5. Kama una fungus miguuni tafuta dawa na uzitibu mara moja, ni hatari harufu miguuni itazidi na hata miguu kuoza.

6. Paka poda (poda za watoto) miguuni kusaidia miguu kuwa mikavu kabla ya kuvaa viatu hasa katikati ya vidole.

7. Pia unaweza kununua spray maalum pharmacy kwa ajili ya kupulizia miguuni na kwenye viatu ili kuondoa harufu.