SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 25 Mei 2017

T media news

HABARI NA HISTORIA YA TANU NA UKOMBOZI WA TANZANIA: MISUKOSUKO NA MABALAA DAR ES SALAAM


SEHEMU YA PILI
Mbali na wasomi pamoja na wanawake, pia jijini Dar es Salaam, vijana wengi wenye nguvu walionekana kukosa muda na harakati za kudai uhuru. Kwani wengi wao walionekana kupenda starehe nyingi kuliko kazi. Wengi walikuwa wakipnda sana kucheza miziki ya kimagharibi huku wakiwa na wanawake wa kizungu. Kitu ambacho wapigania uhuru walipata misukosuko mingi katika kuwashawishi vijana hao kujiunga na mapigano ya kudai uhuru.
Mara baada ya kuona misukosuka kutoka kwa wananchi wenyewe, tugeukie kwenye serikali ya mkoloni ya wakati huo ambayo ni Waingereza waliopewa koloni la Tanganyika kuanzia miaka ya 1919 hadi miaka ya 1960. Hivyo kwa kipindi chote cha kudai uhuru serikali ya kikoloni haikuunga mkono harakati za kuadai uhuru. Hivyo walikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa harakati za WanaTANU zinakomela mbali. Serikali ya kikoloni ilikuwa ikisaidiwa na watu kama Maakida, Maliwali na Machifu. Kwa dare s salaam kulitokea Liwali mmoja aliyekuwa akitumiwa na Wakoloni kwa lengo la kuzuia mikutano ya TANU kufanyiaka jijini Dar es salaam.
Ilifikia wakati  wanachama wa Tanu walikosa mahala pa kufanyia mikutano yao kwani Liwali huyo alianzisha chama chake cha kikabila cha Uzaramo Unity, kwa lengo la kuvunja nguvu za Tanu. Na kama hiyo haikutosha aliuamua kuzuia mikutano ya TANU sehemu zote jijini Dar es Salaam isipokuwa kwenye ofisi za Tanu pale mtaa wa Lumumba. Lakini napo walifukuzwa wakidaiwa kuwa walikuwa wakimpigia kelele Gavana, na hivyo waende kufanyia mkutano wao porini. Porini kwa wakati huo ni maeneo ya uwanja wa taifa kwa kipindi kile kulikuwa na uwanja wa ndege. Ukweli ni kwamba Chama cha Uzaramo Unity kilikuwa na wanachama wengi kwani kilikuwa na nguvu ya fedha. Na kutokana na watu kuona chama kile ni cha kikabila walidhani hata chama cha TANU nacho ni cha kikabila. Na hivyo baadhi ya watu kuona kuwa kuna ukabila na kupuuzia TANU. Lakini bado kulitokea idadi kubwa ya watu kukiamini chama cha TANU.
Haikuishia hapo kwani mkoloni baada ya kuona nguvu ya ukabila inashindikana aliamua kutumia mbinu ya udini. Na mara baada ya wanachama wa TANU kuona hivyo waliamua kuunda kundi lililoitwa Bantu mwaka 1958 na kufanya mkutano mkubwa uliohusisha mashekhe mbalimbali kutoka Lindi wakiwemo wakina Hassan Bin Amir,Mwinyimad Ally na Nurdini. Mkutano huo ulikuwa ukilaani juhudi za wakoloni kutumia dini kuwagawa watanganyika.
Na kipindi hiko hiko wakoloni waliawashawishi baadhi ya watu kuunda chama cha kidini cha AMNUT. haikuishia hapo, kwani miaka ya 1957 ni kipindi ambacho Kenya kulikuwa na vita vya MAU MAU, hivyo wakoloni walitumia dhana hiyo kuwa hata Tanganyika kunaweza kutokaea MAU MAU hivyo wanaTANU wanatakiwa kuacha mara moja harakati za kudai uhuru kwani kutatokea vita. Lakini hiyo haikusaidia kupunguza nguvu za WanaTANU, kwani mnamo mwaka 1957 kulikuwa na ujio wa mjumbe kutoka kwenye chama cha Wafanyakazi nchini Uwingereza bwana John Hatch, ambaye alifanya mkutano pale maeneo ya Mnazi Mmoja na kuunga mkono juhudi za kupigania uhuru. Na hivyo Tanu ilizidi kupata nguvu.