SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 25 Mei 2017

T media news

Sport Pesa Yazikutanisha Tena Simba na Yanga Dimbani..!!!!


Vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga watachuana na timu za Kenya kusaka bingwa wa Ligi ya SportPesa Super Cup.

Ligi hiyo itaanza Juni 5 ambapo Yanga itafungua dimba na bingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, Tusker siku hiyo pia kutakuwa na mchezo kati ya Singida United na AFC Leopards.

Juni 6, Simba itaonyeshana uwezo wa soka na Nakuru All Stars wakati na Gor Mahia itacheza na Jang'ombe ya Zanzibar, mechi zote zikichezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania, Abass Tarimba alisema mashindano hayo yataendeshwa kwa mtindo wa mtoano na fainali itachezwa Juni 11.

"Bingwa ataondoka na kitita cha Dola 30,000  na mshindi wa pili Dola 10,000 na timu zitakazoingia nusu fainali kila moja itapewa Dola 5,000 na timu zote zitakazoshiriki zitapewa kifuta jasho cha Dola 2,500 kila moja," alisema Tarimba.