SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 8 Mei 2017

T media news

Bunge Sports Club yaishinda NMB

Timu ya Bunge Sports Club inayojumuisha timu ya mpira wa miguu, mpira wa pete na kikapu imeibuka washindi na kunyakua vikombe vitatu katika bonanza lililozikutanisha timu ya Bunge na timu ya benki za NMB.


Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati, Abdulmajid Nsekela akisalimiana na mchezaji wa Bunge Sports Club mpira wa Pete ambaye ni Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson kabla ya mchezo wa kirafi wa Pete kati ya Bunge na NMB

Timu ya kwanza ya Bunge kushinda kikombe ilikuwa timu ya mpira wa pete ambayo iliifunga timu ya pete ya NMB magoli 19 kwa 2, ikifuatiwa na timu ya mpira wa kikapu kwa wanaume ambayo iliwafunga wapinzani wao timu ya mpira wa kikapu ya NMB kwa jumla ya vikapu 37 kwa 28.


Wachezaji wa Bunge Sports Club na NMB mpira wa pete wakiwnia mpira wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma

Kikombe cha tatu kwa timu ya Bunge kilipatikana kwa timu ya mpira wa miguu ambayo iliwafunga NMB goli 2-0 na hivyo kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote ambao timu hizo zimekutana.


Meneja wa Kanda ya Kati wa NMB, Straton Chilongala akimkabidhi nahodha wa mpira wa Pete wa Bunge Sports Club ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Esther Matiko

Timu ya Bunge Sports Club na NMB Sports Club zimekuwa zikikutana zikicheza michezo mbalimbali zikiwa na lengo la kuboresha uhusiano baina ya Bunge na NMB ambapo kwa mwaka huu bonanza hilo limefanyika katika uwanja wa Jamhuri uliopo makao makuu ya nchi, Dodoma.


Abdulmajid Nsekela akikabidhi kikombe cha mpira wa Kikapu kwa washindi Bunge Sports Club