Jana jioni wanafunzi 24 wa Shule ya Msingi Butwa walizama ndani ya Ziwa Victori baada ya mtumbwi waliokuwa wakiutumia kuzama.
Wanafunzi 21 wameokolewa katika ajali hiyo ambapo waliosalia watatu hawakuonekana hadi baada ya muda kid0go ambapo miili yao iliopolewa wakiwa tayari wamefariki dunia.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi amesema kuwa wanafunzi hao walikuwa kwenye mtumbwi ambao walikuwa wakiutumia kuvuka walipotoka shule.