Simba imeendelea kuchemsha kwenye uwanja wa CCM Kirumba kila inapocheza na Toto African ya mkoani Mwanza.
Baada ya kupata ushindi wa kukumbukwa (3-2) dhidi ya Mbao FC kwenye uwanja huohuo April 10, 2017, leo April 15, 2017 Simba wameshindwa kupata ushindi dhidi ya Toto African.
Timu hizo zimetoka suluhu baada ya dakika 90 na kugawana pointi mojamoja.
Simba imeshindwa kupata ushindi katika mechi nne za hivi karibuni zilizochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba. Mchezo wa raundi ya kwanza msimu huu Simba walipata ushindi wa magoli 3-0 mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa Uhuru, Dar.
Suluhu hiyo inaifanya Simba kuongeza pointi moja na kufikisha pointi 62 baada ya kucheza mechi 27 huku ikiendwlea kuongoza ligi ikifuatiwa na wapinzani wao Yanga wenye ponti 56 huku wakiwa wamecheza mechi 25 hadi sasa.