SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 15 Aprili 2017

T media news

Rapa Chemical Aweweseka Mwenyewe Suala la Rosa Ree

Kwa muda mrefu msanii Chemical amekuwa ndio Rapa pekee wa kike aliyesimama na kuteka wengi, Ila ujio wa rapa mpya Rosa Ree umekuwa mwiba kwake kwani amekuwa akizunguka kwenye media na kumsema kwa jazba kuwa asilinganishwe nae na hata amemuimba kwenye nyimbo kimafumbo...Kitu ambacho watu wanadhani kuna bifu kati yao, lakini kwa upande mwingine msanii Rosa ree hajawahi sikika kwenye media akimuongelea chochote..Kwa nanivyo ona Mimi Chemical ni msanii mkubwa si wa kutafuta kiki kwa msanii Mdogo kama Rosa Ree , Rosa ndio alipashwa labda kutafuta kiki kupitia Chemical....Alafu namshauri ni vizuri Ku accept challenges , yeye atoe kazi nzuri mashabiki tutabaki kuwa majaji lakini sio kuweweseka itamtoa nje ya reli..
.
Pendaneni jamani mashabiki tunahitaji marapa wengi wa kike zaidi ya ninyi....

By Bahati