SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 15 Aprili 2017

T media news

Mtoto Ampunguza Kilo Uwoya

STAA mwenye mvuto wa kipekee Bongo Muvi, Irene Uwoya amesema amepungua takriban kilo tatu mwilini kutokana na kuugua kwa mtoto wake wa kipekee Krish, mpaka kusababishwa kufanyiwa upasuaji mdogo kitu ambacho kilikuwa kikimnyima raha.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Uwoya alisema mtoto wake alikuwa na tatizo kubwa ambalo hakupenda kuliweka wazi kwenye vyombo vya habari lakini anamshukuru Mungu kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kutibiwa.

“Jamani usisikie kuuguliwa na mtoto, nilikuwa nashindwa hata kula chakula ndiyo maana nimepungua,” alisema Uwoya.