SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 14 Aprili 2017

T media news

Kimenukaa..Jeshi la Polisi Latangaza Vita ..Lajiandaa Kuvamia Mkoa wa Pwani kijeshi Kupambana na Majambazi Walioua Askari..!!!


Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, Nsato Marijani ameongea na waandishi wa habari mchana huu na kutolea ufafanuzi tukio la mauaji ya Askari Polisi 8 lililotokea jana jioni huko Kibiti, Pwani.

CP Marijani ameeleza kuwa tukio hilo sio la kigaidi kama ambavyo imekuwa ikivumishwa, bali ni tukio la kawaida la ujambazi ambalo halililazimu Jeshi la Polisi kuunda Kanda Maalumu ya Kipolisi kwa Mkoa wa Pwani.

Aidha, amesisitiza kuwa, hilo ni tukio la kawaida na wala sio tukio la kutisha na kuzua hofu bali imetokea tu bahati mbaya mapolisi kuuawa na wao kama Jeshi Imara watazidisha mapambano na kudumisha ulinzi.

Mpaka sasa, wameshajibu mashambulizi yaliyowalaza chini majambazi 4 na idadi yao itaongeza kwa kuwa imeundwa operesheni maalumu ambayo haitokuwa na mzaha wala msamaha.

Nikimnukuu CP Nsato Marijani

"Ninasema wazi kwamba hiki ni kitendo ambacho hakikubaliki, mpaka sasa nimekwishapoteza askari zaidi ya kumi. Ninaamini wanatosha.

Kuanzia sasa jeshi linakwenda kwenye operesheni maalumu, hatutokuwa na mzaha wala msamaha, tutafanya kile ambacho Jeshi linapaswa kufanya.

Tutawafuata popote walipo, tutawashughulikia kikamilifu na hakuna ambaye atakayebaki. Na mapambano haya hayana mwisho, yaani huu ni mwanzo hayana mwisho. Askari 10 ni wengi sana.

Wananchi mtuwie radhi, mtuunge mkono. Katika hili mtaona sura halisi ya Jeshi la Polisi

Dawa ya moto ni moto, tuna uhakika tutawakamata, sasa hivi ni nane kwa nne lakini magoli yetu yatakuwa mengi kuliko wao.

Wale wote ambao walikuwa wanafikiria kufanya ujambazi wa aina hii wa kutumia silaha wajue kwamba dawa ya moto ni moto."