SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 15 Aprili 2017

T media news

Kadi tatu za njano zinamkosesha Ndemla mechi ya Toto

Na Zainabu Rajabu

KIUNGO wa Simba Saidi Ndemla atakosekana kwenye mchezo wa leo dhidi ya Toto African kutokana na kuwa na kadi tatu za njano, Ndemla alipata kadi ya tatu ya njano kwenye mchezo wa Jumatatu dhidi ya Mbao FC kwa kumchezea madhambi kiungo wa Mbao Yusuuf Ndikumana.

Hii ni muendelezo wa wachezaji wa Simba kukosekana kwa kutokana na matatizo ya kadi katika michezo ya Mbeya City na Kagera Sugar Simba walimkosa beki wa kimataifa wa Congo Javier Bukungu kutokana na kuwa na kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo dhidi ya Yanga February 25, pia kwenye mchezo wa Jumatatu dhidi ya Mbao Simba walimkosa nahodha wao Jonas Mkude kutokana na kuwa na kadi tatu za njano na sasa ni Said Ndemla.

Makamu Mwenyekiti wa Simba Gogfrey Nyange “Kaburu” ambaye yupo na timu jijini Mwanza amesema: “Ndemla hawezi kucheza kabisa leo kwa sababu ya kuwa na kadi tatu za njano hatutaki kufanya makosa kama waliyofanya Kagera Sugar tutapoteza malengo ya kuchukua ubingwa msimu huu.”

Wakati Simba wakihakikisha hawafanyi makosa kama walivyofanya Kagera Sugar kwa kumchezesha Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano kwenye mchezo dhidi ya Simba na Kagera walishida Kwa mabao 2-1 na kusababisha kupokwa pointi hizo na kupewa Simba.

Pia kikosi hicho kwasasa kinafanya msako kila baada ya mechi kuangalia nani ana kadi nani hana. Jukumu hilo wamepewa watu zaidi ya watatu mojawapo ni kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja.