SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 20 Machi 2017

T media news

Ukweli Mchungu...Mange Kimambi Ndiye Mtu Pekee Anayeweza Kumsafisha Makonda..!!!


Ni ukweli usio pingika kwamba asilimia zisizopungua sitini za watanzania wanaamini kila kitu anachokisema Mange Kimambi kiwe kizuri au kibaya wa tanzania watakichukua kama kilivyo na watakiamini kwa 100%

Nina uhakika 100% Mange Kimambi akiamua kuliyumbisha hili tukio la Bashite kwa kuleta information za kumsafisha Bashite ikiwezekana hata kwa kumchafua Gwajima watanzania watamuamini Mange na shutuma zote ambazo alikuwa anahusishwa nazo Bashite zitakwisha haraka kama moto wa nyasi hii yote ni kwa sababu tu Mange ameshika akili watanzania wengi kiasi kwamba wengine hasa wale wapenda ubuyu ni vigumu sana siku ikapita bila kupitia IG kwenda kuona Mange kaposti nini.

Na kwa kuwa ma bloggers wengi source yao kubwa ya habari ni kwa Mange na kwa kuwa watanzania wengi wanategemea habari kutoka kwenye blogs mbalimbali hivyo basi ina maanisha habari itakayosambazwa itaaminika tu bila kuchujwa wala nini 

Na ukitaka kuamini zaidi kwamba Mange ndio kila kitu ,kuna kipindi alitulia kidogo kupost habari za Bashite ,kutulia kwa Mange kulififisha kabisa habari za Bashite watu walikuwa washaanza kumsahau taratibu na alipoenda kufanya ufunguzi wa barabara alishangiliwa kana kwamba hamna chochote kinacho endelea juu yake.

Hivyo basi napenda kumalizia kwa kusema kuwa sakata la Bashite litaisha pale tu Mange atakapoacha kumuongelea watz watalisahau taratibu taratibu hatimaye wataliacha kabisa

Au kama si kuliacha basi aligeuze juu chini chini juu kwa kutafuta taarifa za uongo na kweli za kumsafisha Bashite na nina uhakika atafanikiwa.