Baada ya kunasa saini ya kiungo mzimbabwe Tafadwaza Kutinyu pamoja na kocha raia wa Uhalanzi Hans van Pluijm, klabu ya Singida United imetangaza kuwasajili wachezaji wengine wawili raia wa Zimbabwe ambao ni Elisha Muroiwa na Wisdom Mtasa.
Singida Unuted ambayo imepanda kucheza ligi kuu Tanzania bara 2017/18 baada ya kufanya vizuri kwenye ligi daraja la kwanza 2016/17 imeanza kusajili mapema ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa VPL.
Katibu wa Singida United Abdulrahman Sima aliwahi kusema, kutokana na uwezo wao wa kifedha klabu yao imejipanga kusajili wachezai watano (5) wa kimataifa kwa ajili ya msimu ujao. Kanuni za ligi kuu Tanzania bara zinaruhusu vilabu vya ligi hiyo kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi saba.