SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 23 Machi 2017

T media news

Nafunga lakini sina mwendelezo mzuri kutokana na majeraha’ – Elius Maguli

Na Baraka Mbolembole

MSHAMBULIZI wa Kimataifa wa Tanzania, Elius aguli ametumia muda mwingi kukaa nje ya uwanja kujiuguza majeraha yake ya kifundo cha mguu lakini bado ameendelea kuwa muhimu katika timu yake ya Dhofar Club katika ligi kuu ya Oman Pro-League.

Maguli tayari amekwishafunga magoli matatu na kutoa–pasi tatu zilizozaa magoli kwa timu yake amepona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu na sasa amerejea uwanjani kuisaidia timu yake iliyo nafasi ya pili nyuma ya Al Shabab kwa alama tano huku michezo minane ikiwa imesalia kabla ya kumalizika kwa msimu.

“Ligi inaendelea vizuri, mpaka sasa tumeshacheza game 18-kwa maana hivi sasa tuko  katika michezo ya mzunguko wa pili na hadi sasa tumeshacheza mechi tano na tumebakiza michezo nane ili kumaliza msimu. Hadi sasa tupo nafasi ya pili nyuma ya Al Shabab kwa tofauti ya pointi tano.” anasema mshambulizi huyo wa Taifa Stars nilipofanya naye mahojiano Jumatano hii.

“Nimefanikiwa kufunga magoli matano na kusaidia mengine matatu. Nimeshindwa kucheza katika michezo mingi kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu na hadi sasa sijafanikiwa kuichezea timu yangu katika michezo miwili kutokana na maumivu haya. Lakini namshukuru Mungu sasa nimeanza mazoezi lakini naweza kusema sikuwa na msimu wenye muendelezo  wa kucheza mfululizo.”