Tarehe 1. Unadhani itachukua mda?hapana,ile tarehe 1 tu inatua kutaanza na Marsesyde derby kati ya mechi kubwa Uingereza ambapo Liverpool watawakarbisha Everton,Ujerumani nako Schalke 04 watawakaribisha Borussia Dortmund moja kati ya michezo inayoangaliwa mno,mbio za uningwa wa Ligue 1 siku hiyo pia zitatoa picha mpya Monaco wakiikabili Psg na kule Ureno miamba miwili Benfica na Fc Porto wataoneshana umwamba.
Tarehe 2.Usiku wa tarehe 1 ukishapita,kunakuja tarehe 2 napo hakuna kulala tunaanza na Serie A,vigogo tishio Napoli watawakabili miamba wasiofungika Juventus mechi itakayoleta taswira ya ubingwa, siku hiyo hiyo Leicester City watakuwa wenyeji wa Arsenal wanaosuasua.
Tarehe 5.Napoli tena na Juventus wataoneshana umwamba katika kombe la nchini humo, Chelsea wanaoukaribia ubingwa msimu huu watapambana na wapinzani wao katika mbio hizo klabu ya Man City,huku kule La Liga Sevilla ambao msimu huu ni tishio kwa vigogo watakuwa Nou Camp kuwakabili Barcelona.
Tarehe 8.Sevilla tena watakutana na miamba mingine katika ligi ya Hispania klabu ya Real Madrid jijini Madrid, lakini hiyo tisa kumi itakuwa Allianz Arena siku hiyo ambapo Bayern Munich watawaalika wapinzai wao wakubwa Borussia Dortmund.
Tarehe 11.Usiku wa Uefa Champions,Juventus watawaalika klabu ya Barcelona nchini Italia hukh Borussia Dortmund nao wakiwa nyumbanj wataikaribisha Monaco,Terehe 12 robo fainali ga pili itapigwa ambapo Real Madrid watakipiga dhidi ya Bayern Munich huku Leicester City wakiikabili Athletico Madrid.
Tarehe 15.Millan Derby,Inter Millan watakuwa nyumbani kuwakabili Ac Millan lakini siku inayofuata yaani tarehe 16 kutakuwa na mechi ya kisasi pale Old Trafford ambapo Mourinho atawakaribisha Chelsea ambao mara zote walizokwishakutana wamemfunga.
Tarehe 18.Robo fainali ya Uefa champions itarudi tena kwa mara ya pili ambapo siku hii Real Madrid wataikaribisha Bayern Munich, Leicester watawakaribisha Athletico Madrid na kesho yake Barcelona watacheza dhidi ya Juventus na Monaco dhidi ya Borussia Dortmund.
Tarehe 22.Chelsea watawakaribisha Totenham Stamford Bridge lakini keaho yake ambayo ni tarehe 23 itakuwa siku ya El Classico na huku kule Uingereza Arsenal wakiikabili Leicester City, Uholanzi nako Psv Eindhoven wataikaribisha Ajax moja kati ya mechi kubwa nchini humo.
Tarehe 26 kinawaka tena Allianz Arena ambapo Bayern Munich watawaalika Borussia Dortmund na siku inayofuata itakuwa ni Manchester Detby huku tarehe 27 ikiwa ni mechi kati ya Tottenham Hotspur dhidi ya Arsenal.