SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 5 Machi 2017

T media news

Mtibwa yenye rekodi mbovu itaweza kuizuia Yanga yenye njaa?

Leo Jumapili March 5, 2017 ligi kuu Tanzania bara itaendelea, lakini mchezo ambao unasubiriwa na macho pamoja na masikio ya wengi ni mechi kati ya Mtibwa Sugar vs Yanga kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Mechi hii inateka watu wengi kwa sababu hendamatokeo yake yakakabadili msimamo wa ligi. Yanga ikishinda mechi hii itaifikia Simba kwa pointi (55) pamoja na idadi ya mechi (24) lakini kubwa kama Yanga itashinda ni kuiondoa Simba kwenye nafasi ya kwanza ya msimamo kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Yanga inahitaji ushindi kwa namna yoyote ile ili kurejea kwenye nafasi ya kwanza kwenye ligi na kuweka hai matumaini yao ya kutetea taji la VPL msimu huu ambalo linawaniwa kwa karibu na wapinzani wao Simba.

Sare ya Simba dhidi ya Mbeya City imewapa mwanya Yanga wa kurudi kileleni endapo watafanikiwa kushinda mchezo wao wa ugenini Morogoro dhidi ya Mtibwa ambayo haijapata ushindi tangu kuanza kwa mwaka 2017.

Kama Yanga itapata matokeo ya sare itafikisha pointi 53 na kuiacha Simba iendelee kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi mbili, lakini ikipoteza mchezo huo Simba itakuwa mbele kwa tofauti ya pointi tatu.

Mara ya mwisho Mtibwa Sugar kuifunga Yanga kwenye uwanja wa Jamhuri ilikuwa ni September 20, 2014 ilipopata ushindi wa magoli 2-0, Je Mtibwa itakomaa kutafuta ushindi wake wa kwanza wa mwaka 2017 kwa kuifunga Yanga?

Takwimu za mechi saba zilizopita zilizokutanisha Mtibwa Sugar vs Yanga, Yanga imeshinda mechi tano, imetoka sare mara moja  na kupoteza mchezo mmoja. Mtibwa imepoteza mechi tano kati ya mechi saba zilizopita dhidi ya Yanga, imeambulia ushindi kwenye mechi moja na kutoka sare mechi moja.

05/03/2017 Mtibwa Sugar ?? Yanga

12/10/2016 Yanga 3-1 Mtibwa Sugar

16/04/2016 Yanga 1-0 Mtibwa Sugar

30/09/2015 Mtibwa Sugar 0-2 Yanga

08/02/2015 Yanga 2-0 Mtibwa Sugar

20/09/2014 Mtibwa Sugar 2-0 Yanga

15/03/2014 Mtibwa Sugar 0-0 Yanga

06/10/2013 Yanga 2-0 Mtibwa Sugar