Tunawaheshimu, timu nzuri, tumepokea , tunajiandaa, saikolojia…wenzetu wako mbali ukilinganisha na sisi
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema wanawaheshimu wapinzani wao kwenye michuano ya Caf Confederation Cup MC Algers ya Algeria kwa sababu ni timu nzuri na inatoka kwenye ukanda wa timu ambazo hufanya vizuri dhidi ya vilabu vya Tanzania.
“Tumeipokea ratiba hiyo na tunawaheshimu wapinzani wetu ni timu nzuri. Wenzetu wametuzidi sana wako mbali kwenye maendeleo ya soka ukilinganisha na sisi lakini tunajiandaa kwa ajili ya kuwakabili, alisema Mkwasa wakati akizungumza na Yahaya Mohamed ‘Mkazuzu’.
Tumejifunza vya kutosha, tutakuwa vzr..mechi hiyo muhimu…ukiwa na timu nzuri unashinda popote nyumbani au ugenini.
Kuhusu Yanga kutofanya vizuri katika michuano ya kimataifa inapocheza kwenye uwanja wa nyumbani, Mkwasa amesema watawaandaa vizuri kisaikolojia wachezaji wao kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mechi ya nyumbani.
“Tumejifunza vya kutosha, tutawaandaa vizuri vijana kisaikolojia kwa sababu tutajiweka pazuri kama tukipata ushindi mzuri kwenye uwanja wa nyumbani.”
Mkwasa amemaliza kwa kusema, ukiwa na timu nzuri unashinda popote iwe ni nyumbani au ugenini.
Yanga imeangukia kwenye kombe la shirikisho Afrika ikiwa ni baada ya kutupwa nje ya michuano ya kombe la mabingwa Afrika, ikifanikiwa kuwatoa MC Alger itafuzu moja kwa moja hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika kwa mara ya pili mfululizo.