SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 21 Machi 2017

T media news

Mchumba wa Amber Lulu Ajitokeza na Kumtambulisha Rasmi...Yabainika Hamorapa ni Muongo


Mkurugenzi wa label ya Kaburu Entertainment, Mr Kaburu weekend hii alifanya sherehe ya birthday yake ambayo iliambatana na kumtambulisha mpenzi wake ‘Amber Lulu’.

Shughuli hiyo iliyohudhuriwa na mastaa mbalimbali wa muziki nchini, ilifanyika nyumbani kwake huko Bunju B jijini Dar es salaam.

Akiongea na ndugu jamaa na marafiki muda mchache baada ya kumaliza shughuli hiyo, alisema ameamua kumtambulisha Amber Lulu kwa jamii ili kieleweke kinachoendela kati yao.

Siku chache zilizopita Hamorapa alijipalilia kuwa anatoka na mrembo huyo mwenye msambwanda wa ukweli kitu ambacho si kweli

Alisema walikuwa kimya kwa muda mrefu kuhusu mahusiano na mrembo huyo kwa kuwa hawakuhafikiana kuweka wazi juu ya mahusiano yao