SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 12 Machi 2017

T media news

Magufuli Awapa Makavu Live Walioimba Wanaimani na Lowassa Mbele ya Kikwete..!!!


Mwenyekiti wa Taifa CCM, Rais John Magufuli amewataka

makatibu wa mikoa wa chama hicho wanaotaka kuingia katika vikao vya

Halmashauri Kuu  (Nec) ya Taifa ya chama hicho wakagombee uenyekiti.

Akizungumza jana (Jumamosi) wakati wa ufunguzi wa kikao cha Nec, Rais Magufuli amesema

kuna watu wanaumuhimu wa kuingia katika vikao vya Halmashauri Kuu na

kwamba wakikosa kutakosekana uwakilishi .

“Nikawaambia mbona mwaka uliopita waliposimama wakimpinga mwenyekiti

makatibu mlikuwepo? Wakati mwenyekiti anawalipa mshahara mbona

hamkumtetea? Mbona hamkusimama kupigana na bado wakaendelea  kuimba

wanaimani na mtu fulani na wengine mkawa mnaitikia,”amesema.

Amesema kwa kuwa mabadiliko ya Katiba na Kanuni ambayo yatapunguza

idadi ya wajumbe wa vikao vya juu vya chama hicho walishayajadili

katika  kikao kilichofanyika Desemba 13 mwaka jana, ni matumaini yake

kuwa kikao hicho hakitachukua muda mrefu kuyajadili.