SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 8 Machi 2017

T media news

KWA DELAY TECHNIQUE (MBINU YA UCHELEWESHAJI) HII MBUNGE WA BUNDA MJINI UMETUKOSEA WAPIGA KURA WAKO OMBA RADHI


Kuna msemo wa Kiswahili unasema kwamba “ukiwa muongo usisahau”,siku za hivi karibuni takribani siku mbili hivi tangu tarehe 07.03.2017 mbunge wa jimbo la bunda kwa nyakati tofauti amejipambambanua kuwa “amefanya kile ambacho hakijawahi kufanywa na mbunge yeyote wa jimbo hilo(Bunda) kwa kugawa vitabu kwa shule za jimbo hilo ”

Mimi nakubaliana na wote na naunga mkono jitihada za mtu yeyote kushiriki katika ukuaji na uchangiaji wa Elimu mahali popote katika nchi hii na hususani jimbo la bunda.Lakini naomba nifafanue mambo mawili ambayo yanaondoa uhalali wa kile alichokifanya mbunge huo na kukionesha kupitia ukurasa wake wa facebook https://web.facebook.com/ester.bulaya/posts/1325509964138713  namtaka atuombe radhi wapiga kura

Kwanza si kweli kwamba mbunge huyo amegawa vitabu kwa shule zote sa serikali na binafsi ,na kwa kuzingatia hilo ukiangalia mabox yanayoonekana katika post yake hayaoneshi kutosheleza maelezo yaliyowekwa kwenye ukurasa wa jamii forum https://www.jamiiforums.com/threads/ester-bulaya-agawa-vitabu-vya-michepuo-ya-sayansi-na-sanaa-kwa-shule-zote-katika-jimbo-la-bunda.1212404/page-6  kwa lengo la kukazia kile alichokifanya mbunge huyo,ukweli ni kwamba kwa jimbo la bunda lenye shule za sekondari 16 ambapo 10 ni za serikali na 6 ni binafsi ,pia jimbo lenye idadi ya shule za msingi 66 ambapo 61 ni za serikali na 5 ni za binafsi huwezi kuuaminisha umma wa watanzania kuwa kwa wale waliofika kupokea ni wawakilishi wa wengine ,

Kwa wasioifahamu jiografia ya Bunda mjini yenye kata 14 kutoka kwenye kata moja hadi ofisi ya mbunge ni umbali usiozidi dakika 60 yaani saa moja.,sasa iweje upige picha na watu (walimu ) 6 halafu ujipambanue kuwa umegawa vitabu kwa shule za jimbo zima?,hakuna mahali popote ambapo anaonesha kuelezea kuwa hao alipiga naopicha ni wawakilishi tu kwa kudanganya huku namtaka atuombe radhi wapiga kura  na wana jimbo wa bunda mjini.

Pili ni ujanja aliotumia na hasa mbinu ya kisiasa inayoitwa (delay technique) mbinu ya ucheleweshaji ambapo kama mtakumbuka Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ambaye pia ni mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa mara tarehe 21.09.2016  alikabidhi vitabu vya sayansi na hesabu  elfu 25, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500 kwa Wabunge wote wa Mkoa wa Mara kwa ajili ya shule za msingi na sekondari mkoani humo.

Makabidhiano hayo yalifanyka katika uwanja wa Mukendo uliopo Musoma Mjini Mkoani Mara na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Nnano pamoja na wananchi mbalimbali waliofika katika uwanja huo ili kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

Wabunge waliokabidhiwa vitabu hivyo ni Marwa Ryoba jimbo la Serengeti (Chadema) ambaye pia ni katibu wa umoja  wa wabunge wa mkoa wa mara, Wabunge wengine waliokuwepo kwenye makabidhiano hayo ni Ester Matiko (Tarime Mjini, Chadema), John Heche (Tarime Vijijini, Chadema), Boniphace Mwita (Bunda Vijijini, CCM), Kangi Lugora (Mwibara, CCM) na ambao hawakufika akiwemo mbunge wa bunda mjini  walituma wawakilishi ambapo katibu wake alipokea kwa niaba. Taarifa hiyo inapatikana  https://michuzi-matukio.blogspot.com/2016/09/profesa-muhongo-awakutanisha-wabunge-wa.html

Sasa kwa kitendo cha mbunge kuchelewa kuvigawa vitabu ambavyo kimsingi hakutoa hata shilingi kumi kuvinunua na vimetolewa kwa hisani ya mbunge wa musoma vijijini baadae kutaka sifa ili aonekane yeye ndio kafanya hivyo ametukosea sana wapiga kura anapaswa kutuomba radhi.

MBUNGE WA BUNDA MJINI TUOMBE RADHI WAPIGA KURA

Wasalaam

#WatumbuaMajipu