SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 20 Februari 2017

T media news

Yanga yashindwa kuomboleza kifo cha mchezaji wake Bonny, TFF yaingilia kati


Kumekuwa na minong’ono mingi kwenye mitandao ya kijamii mjadala ukiwa ni kuhusu Yanga kutosimama kwa dakika moja wala kuvaa vitambaa vyeusi mikononi wakati wa mechi yao dhidi ya N’gaya Club kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Geoffrey Bonny mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania.

Yahaya Mohamed ameongea na Alfred Lucas kujua kama TFF walikuwa wanahusika kuhakikisha kunakuwa na dakika moja ya kusimama na kukaa kimya pamoja na wachezaji wa Yanga na benchi la ufundi kuvaa vitambaa veusi au ulikuwa ni uzembe wa Yanga kama watu wanavyozungumza.

“Meneja wa Yanga Hafidh Saleh alimuomba match commissioner Monnyenyone Nhlapo kumpa taarifa kwamba wanaomba dakika moja ya kukaa kimya na kuvaa vitambaa vyeusi kwa ajili ya kumuenzi mchezaji wao wa zamani Geoffrey Bonny aliyefariki hivi karibuni na alikuwa anazikwa siku ambayo Yanga walikuwa wanacheza mchezo wa kimataifa dhidi ya N’gaya Club ya Comoro.”

“Match commissioner alikubali hilo jambo , nikamuomba mimi nikawape taarifa hiyo waamuzi lakini akasema nisiende mimi jukumu hilo atalifanya yeye, kwaku yeye alikuwa msimamizi wa mchezo sisi wengine tukawa hatuna maneno.”

“Naomba TFF isilaumiwe, wala Yanga ila alaumiwe match commissioner kwa sababu alikubali kwamba atakwenda kutoa taarifa kwa lakini hakutoa hiyo taarifa, kwa kweli jambo hilo linahuzunisha kwa sababu Yanga hawakusimama hata kwa dakika moja wala kuvaa vitambaa vyeusi kuomboleza kifo cha mchezaji wao wa zamani.”

“Meneja wa Yanga alifanya kazi yake vizuri, alitoa taarifa saa nane siku ya mchezo japo ilikuwa imechelewa na haikujadiliwa siku ya kikao cha pre-match meeting, lakini aliwahi kutoa taarifa siku ya mchezo na tukajadiliana kwenye kikao cha ghafla na match commissioner akakubali lakini mwisho wa siku hakuwaambia waamuzi ndio maana hawakutekeleza.”

Kabla ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Azam vs Mwadui kulikuwa na ukimya wa dakika moja kutoa heshima kwa Bonny ambaye alikuwa mchezaji wa ligi kuu na aliwahi kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania.