Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewakingia kifua mastaa waliotuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, akieleza kuwa busara inahitaji katika kupambana na vita hiyo.
Licha ya kuunga mkono jitihada za serikali kupambana na biashara hiyo haramu, Nape amedai kuwa kuwatuhumu mastaa bila kuwa na uthibitisho ni kubomoa ‘brand’ zao walizohangaika kuzitengeneza kwa miaka mingi.
“Kutengeneza brand ni kazi kubwa sana, kuibomoa brand inaweza kuwa ni jambo la siku moja, tena la sekunde,” Nape amewaambia waandishi wa habari Jumapili hii.
“Kusema bana huyu kichaa the brand is destroyed. Lakini lazima kukaa chini kufikiria kwamba mwisho wa siku tunataka tupate matokeo gani. Ni vizuri kuliangalia tunalifanya katika namna ambayo inalinda haki ya mtuhumiwa ya kumpa room ya kesho na kesho kutwa kama ikithibitika kwamba hahusiki bado aliregain brand ama heshima ambayo atakuwa ameitengeneza,” aliongeza.
“Suala la njia iliyotumika niiache public ijadili na itaamua. Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kwahiyo hawajabiki kutuuliza, akitaka anaweza kutuuliza. Lakini kwamba tulihusishwa hatukuhisishwa.”
Wema Sepetu, Vanessa Mdee, Mr Blue, TID ni miongoni mwa mastaa waliotajwa kwenye orodha ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.