SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 16 Februari 2017

T media news

UVCCM TAIFA WAFIKIRIA KUIBADILISHA VIJANA JAZZ BAND KUWA CHUO CHA MUZIKI

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka kwa nyakati tofauti leo 15 Februari amekutana na kufanya mazungumzo na wasanii wa muziki nguli hapa nchini akiwemo Msanii Banana Zoro na msanii mwanadada Stara Thomas waliomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya UVCCM, Jijini Dare es Salaam.

Katika mazungumzo yake na wasanii hao nguli na wenye mafanikio makubwa nchini katika medani ya mziki Kaimu Katibu Mkuu alipokea Ushauri na namna bora zaidi ya kuboresha bendi ya UVCCM VIJANA JAZZ BAND wana “Saga rumba” ambayo hufanya maonesho yake kila siku ya Jumapili eneo la Vijana Social Kinondoni.

Hata hivyo, katika mazungumzo hayo, wote kwa pamoja wameahidi ushirikiano mkubwa katika maboresho makubwa na stahiki kwa bendi ili sasa ijiendeshe kitaalam.

“Vijana jazz ni bendi iliyojijengea heshima miaka mingi hivyo ni tuna kila sababu ya kuimarisha ili iweze kujitangaza na kufikia mafanikio kulingana na mahitajio ya muda tuliona ” alisema Banana.

Kwa upande wake Stara Thomas katika maongezi yake na Kaimu katibu mkuu alisema “Hii ni bendi inayopaswa sasa kuwa chuo cha muziki kwa vijana waje wajifunze mziki na kusambaa kwingineko”

Katibu mkuu Ameahidi kufanyia kazi ushauri uliotolewa kwake na wanamuziki hao kwa ukizingatia kauli mbiu ya CCM Mpya Tanzania Mpya sambamba na kuongeza soko la ajira kwa vijana kupitia mziki wa dance.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka akiwa katika mazungumzo hayo

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka akifanya mazungumzo na msanii BananaZorro