SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 16 Februari 2017

T media news

UFUGAJI WA RASTA WAGEUZWA BIASHARA MJINI.



Dar es Salaam. Imebainika kuwa watu hufuga nywele aina ya rasta maarufu kama ‘dread’ kisha kuwauzia watu wengine kati ya Sh150,000 hadi Sh1milioni, kulingana na ubora.

Nywele hizo zinapouzwa watu huzinunua na kuunganisha na zao, mfano mtu anayetaka kuwa na rasta lakini ana nywele fupi anaenda saluni au kwa mtu mwenye rasta ndefu ambapo huuziwa kulingana na urefu anaotaka.

Ukweli wa mambo yote anauleza Furaha John mkazi wa Segerea wilayani Ilala, mwenye nywele aina ya rasta vipande 220 alizozikuza kwa muda wa miaka saba ambazo anaziuza kwa bei ya Sh7,000 kwa kipande kimoja  chenye urefu wa sentimita 15.

“Ndiyo dada (mwandishi) mimi nauza nywele zangu na hapa tayari nina oda ya watu wawili, nywele zangu naziuza kwa vipimo, napima saizi ya kidole gumba (anaonyesha akipima nywele zake kwa kurefusha kidole gumba  na kidole kingine urefu unaokaribia  sentimita 15).

Furaha ambaye rasta zake ni ndefu zinafika katikati ya mgongo, alisema anatarajia kujipatia faida ya zaidi ya Sh3 milioni atakapoziuza.