Msanii wa Bongo Fleva Nay wa Mitego ameiambia eNewz ya EATV kwamba hajawahi kutengeneza kiki ila kiki ndiyo zinamfuata kwa kuwa yeye ni msanii anayependwa kusikilizwa kuliko msanii yeyote.
Kuhusu sekeseke la mwaka jana lililohusisha kutupiana madongo kati yake na Niva, amesema kuwa Niva alidanganya aliposema wapanga kufanya jambo hilo kwa ajili ya 'kiki' huku akikanusha kuwa hakuwahi kabisa kutengeza kiki na msanii huyo wa bongo movie.
“Mimi sitengenezi kiki bali kiki zinanifuata na nitake radhi sijawahi kufanya kitu kama hicho na mtu kama yule na ninapa kwa Mwenyezi Mungu na Mungu wangu anayenisikiliza sijawahi kutengeneza kiki na mtu wa dizaini ile biashara yangu na yeye haziendani mimi nafanya muziki”
Mwaka 2016 Niva alidai kuwa Nay alim-diss kwenye ngoma yake kwamba hana nyumba na wala hana sehemu ya kulala bali analala kwenye gari jambo ambalo lilizuia vita ya maneno kati ya Nay na Niva