SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 18 Februari 2017

T media news

POLISI AFUNGUKA KWANINI DIAMOND PLATNUMZ HAKUFIKISHWA MAHAKAMANI

Mohamed Mpinga ni Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania na amekubali kukaa kwenye Exclusive Interview na AyoTV kujibu baada ya watu ku-comment kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuona Diamond amepost picha akiwa na Kamanda na hakupelekwa Mahakamani.

Kamanda Mpinga ameeleza kwanini Mwimbaji Diamond Platnumz hakupelekwa Mahakamani baada ya video yake kusambaa akiendesha gari huku akiimba na kucheza wakati kuna wale wa Singida walipelekwa mpaka Mahakamani kwa kosa hilohilo.