Mwanajeshi wa Israel ambaye alimuua mshambuliaji Mpalestina ambaye alikuwa tayari amejeruhiwa amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela.
Sajini Flor Azaria alipatikana na hatia ya kuua kwa kumpiga risasi Abdul al-Sharif mwenye umri wa miaka 21 eneo linalokaliwa na Israel la Ukingo wa Magharibi Mwezi Machi.
Azaria alikuwa amemwambia mwanajeshi mwenzake kwa Sharif ambaye alikuwa amemchoma kisu mwanajeshi mwingine kuwa alistahili kufa.
Makamanda wa jeshi walilaani kitendo chake huku wengine wakimpongeza.
Hukumu kwa makosa kama hayo ni miaka 20, lakini waendesha mashtaka walikuwa wakitaka Azaria kufungwa kati ya miaka mitatu na mitano.
Familia ya Sharif nayo ilikuwa inataka Azaria kupewa kifungo cha maisha jela.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema kuwa anaungua mkono uamuzi wowote wa kumsamehe Azaria.
Mauaji hayo yaliangaziwa pakubwa baada ya kisa hicho kilichorekodiwa kwa simu na kupeperushwa na televisheni za Israel.
Mahama iliyosikiliza kesi hiyo ilitupilia mbali madai ya Azaria kuwa alikuwa na hofu, akidhani kuwa Sharif alikuwa amejifunga vilipuzi.