SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 15 Februari 2017

T media news

MISS TANZANIA 2010, GENEVIEVE ADAI HANA MPANGO WA KUDATE NA MSANII

Miss Tanzania 2010 Genevieve Emamanuel ambaye kwa sasa ameingia rasmi kwenye game ya muziki akiwa tayari ameshaachia ngoma yake iitwayo ‘Nana‘ ambapo ukiweza kusikiliza ngoma hiyo vizuri basi hakika uwezo wake katika uimbaji utakushangaza.

Genevieve ameweka wazi kuwa hawezi kuwa na mahusiano na mtu ambaye anafanya muziki kama yeye kwakua anahofia migongano ya kimslai. Genevieve alidai kwa sasa bado hana mpenzi.

Genevieve

Kupitia kipindi cha Twenzetu cha Times Fm alisema, “Mimi natamani kuwa na mwanaume ambaye si mwanamuziki kwakua nahitaji mtu ambaye yupo tofauti ili kuepuka migongano ya kimaslai hivyo nadhani mimi kuwa na mtu ambaye ni msanii itakua sio vizuri, so nahitaji mtu lakini napenda awe mtu ambaye ataelewa na kuthamini ninachokifanya”.

Aidha Genevieve amesema kuwa kitendo cha kuwa karibu na jamii kimemfanya aendele kubaki kwenye maskio ya watu na kimefanya muziki wake upokelewe vizuri na watu.

“Si watu wengi walikuwa wananisikia ila kitu ambacho kilikuwa kinanifanya niwe maskioni mwa watu nadhani ni uwezo wangu wa kuwa karibu na jamii hivyo sikupotea ila nilikuwa najitahidi kuwa karibu na wanajamii na nashukuru sana kwakua watu wamenipokea vizuri nannyimbo yangu hii”