Image captionMgombea wa Uholanzi Geert Wilders
Mwanasiasa wa Uholanzi, Geert Wilders, anafanya mkutano wa mwanzo wa kampeni yake, na anahisi kuzuwia Waislamu kuhamia nchini humo, na kwamba atafunga misikiti.
Vilevile amawataja raia wa Morocco kuwa kashfa
Ulinzi mkali umewekwa katika mkutano huo karibu na Rotterdam.
Umebaki mwezi mmoja kabla ya uchaguzi, na kura za maoni zinaonesha kuwa chama cha bwana Wilders kina uongozi mdogo, ikilinganishwa na kile cha waziri mkuu, Mark Rutte.
Lakini katika majuma ya karibuni, wafuasi wa Bwana Wilders wamepungua.
Mwandishi wa BBC nchini Uholanzi, anasema kwa vile Bwana Wilders anamuunga mkono Donald Trump, inaonesha amepoteza baadhi ya wafuasi.