Kwenye historia za wazazi wengi wa kike ukifatilia utagundua mara nyingi ndiyo huwa karibu zaidi na familia au watoto wao,Mama mzazi wa msanii JUX anaingia kwenye headlines za Bongo kwa kuhudhuria show ya kwanza ya mtoto wake ‘Jux’ toka aanze kufanya muziki wa bongo fleva.
Show ya Love,Melodies &Lights iliyofanyika wikiendi iliyopita, miongoni mwa wahudhuriaji alikuwa ni pamoja na Mama yake Jux,na amekubali kusema ya moyoni baada ya kufika>> ’Namuonaga kwenye TV tu, nimejisikia furaha mpaka nimechanganyikiwa sijawahi kumuona live’
‘Kiukweli anajitahidi sana nimefurahi,tumuombee azidi kufanya vizuri,Nilikua namuona kwenye Macd cd,Nyimbo zake ni za uchangamfu sana akiwa jukwaani’ – Mama yake Jux.