SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 14 Februari 2017

T media news

Luis Enriue Awaonya Wachezaji Wake Juu Ya PSG.

Kocha wa Paris Saint-Germain, Unai Emery atatumia uzoefu wake uliopita dhidi ya Barcelona kwenye mchezo wao wa leo, amesema kocha wa Barcelona Luis Enrique.

Vilabu hivyo viwili vinakutana kwenye uwanja wa Parc des Princes ukiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya klabu bingwa Ulaya.

Barcelona iliwaondoa PSG kwenye hatua ya robo fainali mwaka 2013 na 2015 za shindano hili, lakini kocha mkuu wa Barcelona Enrique ametoa tahadhari kwa wachezaji wake kuwa PSG “wana muunganiko zaidi kwa sasa.”

‘Anatufahamu vyema sana, na pia anajua fika ni kitu kipi tutakifanya uwanjani.

‘Lengo letu ni kukaa na mpira zaidi na kuweka nafasi au pengo kwa sababu lazima watataka kujilipua kwa kiasi fulani.

‘Kwa sasa wananyumbulika zaidi kuliko kipindi kilichopita, wana muunganiko bora na washambuliaji wao ni hatari pia’.

Wakati Barca watakuwa wanaweza kutegemea ubora na maajabu ya Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar, PSG watamtegemea mshambuliaji raia wa Uruguay  Edinson Cavani, aliyekuwa kwenye fomu bora zaidi pengine ya maisha yake akiwa amefunga mabao 25 kwenye ligi msimu huu, huku pia akiwa maetoa assist 9 katika michezo 6 iliyopita.