SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 14 Februari 2017

T media news

ARUSHA: Askari Polisi Ashikiliwa kwa Kujihusisha na Dawa za Kulevya...!!!


Jeshi la polisi mkoani Arusha linawaashikilia watuhumiwa 14 na jumla ya kete 167 za madawa ya kulevya aina ya HEROIN. Mbali na watuhumiwa hao wa madawa ya kulevya misako hiyo ilifanikisha kukamata madawa ya kulevya aina ya mirungi kilogram 33 pamoja na watuhumiwa 12

Pia kamanda wa polisi ameeleza kuwa tangu kuanza mwezi huu wa pili jeshi la polisi limekuwa likifanya misako mbali mbali katika Bara Bara, mitaa na vitongoji mbali mbali ndani ya wilaya zote za mkoa huu wa Arusha ambapo jumla ya misokoto 3845 ya bangi ilipatikana na jumla ta watuhumiwa 54 walikamatwa na kufunguliwa kesi katika vituo mbali mbali vya polisi.

Kati ya watuhumiwa hao waliokamatwa na Bangi Kuna wauzaji wa madawa hayo ambapo idadi Yao Ni 40, msafirishaji mmoja na Askari mmoja kwenye namba za kijeshi F.6978 D/CPL ZAKAYO ambae nae anashikiliwa huku uchunguzi dhidi yake ukiendelea kufanyika.

Jumla ya watuhumiwa 12 wa mirungi na 14 wa heroin wote wana makosa ya kupatikana na madawa hivyo kufanya jumla ya watuhumiwa wote kufikia 80.