SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 15 Februari 2017

T media news

HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA TID KWENYE BIRTHDAY YA RC MAKONDA

Ikiwa Jumatano hii ni siku ya sherehe ya kuzaliwa kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, TID ni miongoni mwa mastaa wa kwanza kumpongeza kiongozi huyo wa serikali japo wiki chache zilizopita aliingia matatani baada ya kutajwa kwenye orodha ya kwanza ya majina ya wanaohusika na madawa ya kulevya.

Kupitia mtandao wa Instagram, muimbaji huyo ameweka picha ya Makonda na kuandika, “Happy Birthday Daresalaam,happy birthday Mheshimiwa…. @paulmakonda am so happy today.”

Kwa sasa TID na Makonda wanaonekana kuwa karibu huku siku chache zilizopita muimbaji huyo alitembelea nyumbani kwa kiongozi huyo akionyesha kuwa ameamua kubadilika na kumuunga mkono katika vita ya kupambana na madawa ya kulevya.

Pia TID alimake headlines Jumatatu pale alikiri kuwa mwathirika wa madawa ya kulevya kwenye mkutano ulioandaliwa na mkuu huyo wa mkoa.