SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 3 Februari 2017

T media news

HAJI MANARA ASHWINDWA KUMPOSA WEMA SEPETU BAADA YA HAYA


Hatimaye Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Sunday Manara atashindwa kumposa mnyange Wema Sepetu, baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupangua tena ratiba ya ligi kuu, kwa kusogeza mbele mchezo wa Azam na Ndanda FC.

Mchezo huo uliokuwa umepanga kufanyika Jumamosi ya Februari 4, sasa utafanyika Jumapili Februari 5 ili kutoa nafasi kwa Azam FC kujiandaa vizuri kutokana na timu hiyo kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, siku ya Jumatano usiku.

Maamuzi haya yamefanyika ikiwa ni takriban siku 10 tangu Msemaji huyo wa Simba Haji Manara atangaze kumposa aliyewahi kuwa Miss Tanzania, ambaye pia ni nyota wa bongo movie Wema Sepetu, endapo ratiba isingepanguliwa tena.

Manara alisema kuwa alikuwa na uhakika kuwa ni lazima ratiba ingepanguliwa tena, mara baada ya TFF pia kupangua tarehe ya mchezo kati ya Simba na Yanga uliosogezwa kutoka Februari 18 hadi Februari 25 huku akionesha kushangazwa na jinsi ambavyo TFF inashindwa kutengeneza ratiba ya uhakika.

Katika taarifa yake aliyoitoa usiku wa Januari 23 mwaka huu, manara alisema  "Iwapo Kama ratiba yao ya Ligi kuu na Kombe ila shirikisho haitabadilishwa kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu, ntamposa mlimbwende Wema Sepetu, na akikubali ntamuoa, akikataa ntatembea na boxer toka Nyumbani kwangu hadi TFF" 

Kwa mabadiliko haya ambayo sasa TFF imeyatanga, ni dhahiri kuwa hakuna ndoa tena kati ya Manara na Wema Sepetu, isipokuwa tu kama atatangaza vinginevyo.