SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 22 Februari 2017

T media news

Godzilla Ajiita Mfalme wa Mitindo Huru 'Freestyle' Bongo.

Rapa Godzilla kutoka Salasala amejitangaza rasmi kuwa yeye ni mfalme wa Freestyle bongo na kusema jambo hilo halina ubishi wowote ule kwani Marapa wengi hapa Bongo hawajui kufreestyle.

Godzilla ameandika “Rasmi…Mimi ndiyo mfalme wa Mitindo huru Bongo” kupitia mtandao wake wa twitter na kudai hakuna rapa ambaye anaweza kufanya mitindo huru kama yeye, akitaja kigezo alichotumia ni kutokana na baadhi wa Marapa kushindwa kutunga mistari yenye maana wakati waki freestyle na badala yake wanajikuta wanarudia mistari ambayo walishawahi kutumia kwenye nyimbo zao za awali.
Huenda Godzilla amepigilia msumali wa chaguo la Rapa Young Killer ambapo jana wakati akihojiwa na kituo cha East Africa Radio alitaja Marapa ambao anawakubali kwa mitindo huru (Freestyle) kuwa ni Godzillah na Nikki Mbishi ingawaje alikuwa anavutiwa zaidi na marehemu Albert Mangwea.