SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 16 Februari 2017

T media news

DR Congo haitafanya uchaguzi wa Rais tena

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imesema haitoweza kumudu gharama za uchaguzi wa Rais uliokuwa umepangwa kufanyika mwaka huu, serikali imesema.

Waziri wa bajeti, Pierre Kangudia amesema gharama za kuendesha uchaguzi ambazo ni dola bilioni 1.8 ni kubwa mno. Mwaka jana, serikali na upinzani vilikubaliana kufanya uchaguzi mpya mwishoni mwa mwaka huu.

Utawala wa Rais Joseph Kabila ulimalizika November 2016. Wapinzani wa Kabila wamemshutumu kwa kuendelea kuchelewesha uchaguzi ili aendelee kukaa madarakani.

Kabila aliingia madarakani mwaka 2001 baada ya kuuawa baba yake, Laurent Kabila.