Mwanamama Angelina Jolie alishindwa kuzuia hisia zake na kuanza kulia alipokuwa akihojiwa kwa mara ya kwanza juu ya kuvunjika kwa ndoa yake na mkali wa Movie Brad Pitt.
Mwanamama huyo alitoa ya moyoni wakati wa mahojiano na kituo cha televisheni cha BBC alipokuwa nchini Cambodia na familia yake wakati wa kuipimia kwa mara ya kwanza movie yake mpya ya ‘FIRST THEY KILL MY FATHER’
“Sipendi kuongelea sana jambo hilo ila nataka niseme kuwa kilikuwa ni kipindi kigumu sna kwenye maisha yangu kama binadamu wa kawaida. Tulikuwa familia na naamini tutalivuka hili kama familia na tutakuwa imara zaida kutokana na hili lilotokea” Alisema Angelina Jolie.
Wawili hao walifunga ndoa miaka mitatu iliyopita, lakini walikuwa pamoja kwa zaidi ya muongo sasa. Wamekuwa pamoja tangu mwaka 2004 na wana watoto sita, Maddox, Pax, Zahara, Shiloh, Vivienne, na Knox.