Msanii Alikiba ambaye leo ameachia remix ya wimbo wake wa 'Aje' ameonesha kumkosha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kiasi cha Waziri huyo kusema kuwa Alikiba ni kati ya wasanii wanaofanya ajisikie fahari kuwa Waziri
Mhe. Nape Nnauye amesema hayo leo baada ya msanii huyo kukabidhiwa tuzo yake katika kituo kimoja cha Television nchini Afrika Kusini na kuachia kazi yake mpya ambayo imeonesha kuwakosha watu wengi.
"Kiba! Big Up! Am so proud of you! we ni mmoja wa wasanii wanaonifanya nijisikie fahari kuwa Waziri wa Sanaa Tanzania! May allah bless you!" aliandika Nape Nnauye
Msanii Alikiba ni kati ya wasanii wachache kutoka Tanzania ambao wanaiwakilisha vyema nchi kupitia muziki wao.