Jana kupitia page yake ya Inatsagram rapper Nikki Mbishi alitusanua kuwa siku chache zilizopita alipokea ujumbe wa maandishi (SMS) kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Ujumbe ambao ulimtaka rapper huyo kuhudhuria ofisini kwao mapema Ijumaa ya February 10 ili kuzungumzia mustakabali wa wimbo wake wa “I’m Sorry JK”.
Kupitia page yake ya Instagram rapper Nikki Mbishi alipost picha yenye maneno iliyoambatana na caption iliyosomeka kama ifuatavyo.
“Salaam Tanzania,Afrika na Dunia! Leo tarehe 13/02/2017 nimehitajika kuripoti ofisi za BASATA ambapo wanadai walinitumia ujumbe zaidi ya siku 3 nyuma ila sikuwa hewani labda kwa sababu ya msiba ulionipata, kufuatia ujumbe niliyotumiwa juzi tarehe 09/02/2017 kwa njia ya msg za kawaida za simu ya kiganjani ambapo ujumbe umesema hivi “Habari za jioni?Tafadhali fika bila kukosa BASATA kesho 10/02/2017 saa tatu kuzungumzia mustakabali wa wimbo wako wa ” I AM SORRY JK” Nimeomba niripoti leo kufuatia kuchelewa kufika kwa ujumbe huo. Unadhani nini kitatokea?Mi sifahamu ninachofahamu ni Itika wito kataa neno. Asanteni na Mungu awabariki nyote. #TagWaTanzania #TagWaTanzania #TAGVIUMBEHAIWOTE #TAGVIUMBEHAIWOTE”
Kwa maana hiyo inaonyesha dhahiri kuwa lipo ambalo BASATA wameliona katika wimbo mpya wa Nikki Mbishi unaoitwa “I’m Sorry JK” cha msingi ni kusubiri matokea kama alivyodai Nikki Mbishi.