SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 25 Januari 2017

T media news

Timu 7 zimeshantangulia robo fainali..zinasubiriwa mbili leo.

Herve Renard ni mtemi bwana!Aliwapa ubingwa Ivory Coast Afcon iliyopita na jana akawatoa katika mashindano hayo.Kocha huyo safari hii yuko na Morocco jana aliitembezea kichapo cha bao moja kwa bila timu yake hiyo ya zamani na kuwatoa katika mashindano.DR Congo nao wamewatoa Mali na hadi sasa kuzifanya timu zilizofuzu hatua inayofuata kuwa timu saba.Leo kuna timu moja kati ya Egypt na Mali itaungana na hizo timu 7 ili kukamilisha 8 za robo fainali.

Ghana tayari wameshafuzu katika hatua ya robo fainali na mchezo wao wa leo dhidi Misri ni wa kukamilisha ratiba kwao.Hata Ghana wafungwe na Misri bado watafuzu katika hatua ya robo fainali kwani watabaki na pointi 6 huku Misri ataongoza kundi kwa pointi 7.Lakini huu ni mchezo wa lazima kwa Misri kupata angalau hata pointi 1 ambayo itawafanya kufikisha pointi 5.Pointi 5 haziwezi kufikiwa na Mali kwani wakishinda mchezo wao dhidi ya Uganda wataishia pointi 4.Lakini Ghana nao watahitaji kumaliza kwa kuongoza kundi hili hivyo hautakuwa mchezo rahisi kwa Misri.

Uganda nao hawajapata ushindi katika mechi hata moja.Huku golikipa wao Dennis Onyango ikifikiria kustaafu timu ya taifa baada ya mchezo wao wa leo.Uganda watahitaji angalau kupata ushindi mmoja katika mashindano haya ili kuondoka walau na heshima kidogo kurudi nyumbani.

Mali nao wanahitaji sana pointi 3 dhidi ya Uganda kwani wakishinda mchezo wao wa leo na huku Ghana akamfunga Misri watalingana kwa idadi ya pointi na Misri na hivyo mmoja wao atafuzu kwa idadi ya magoli.Hii nayo haiwezi kuwa mechi rahisi kwa Mali ukizingatia kwamba Micho ni ngumu kuondoka kwa fedheha bila pointi hata moja.Uganda wasipopata pointi leo itakuwa ndio timu pekee katika Afcon 2017 kuondoka bila pointi hata moja.

Sasa hapa utamu wa Afcon 2017 unazidi kunoga.Channeli yako ya ZBC2 itakuletea moja kati ya mapbano hay na likiisjlha tu wanakuwekea marudio ya pambano lingine.Nani ataungana na Ghana Group D?usikose kuangalia ZBC2 saa nne kamili usiku.