Kwenye interview na jarida la Rolling Stone Mtoto wa Pop Star Michael Jackson ‘Paris Jackson‘ amesema anaimani baba yake aliuwawa.
Paris Jackson anasema “Nani imani kuwa baba yangu aliuwawa na kifo chake kilipangwa ila nikiongelea jambo hili linaonekana ni stori isiyokuwa na vithibitisho vya kutosha,sito kata tamaa“.
Alipoulizwa nani alitaka kumuuwa baba yake, Paris alisema ‘Watu wengi tu“.
Paris-Michael Katherine Jackson mwenye miaka 18 sasa alimpoteza baba yake akiwa na miaka 11.
Michael Jackson alifariki June 25, 2009 sababu ya ikitajwa kuwa ni kiasi kikubwa cha dawa ya propofol kwenye mwili wake.
Daktari wake Dr. Conrad Murray, alikutwa na hatia ya kusababisha kifo cha MJ na kwenda jela kwa miaka 2 na miwili mengine alitumikia nje.