Kiungo mlinzi wa Azam FC Himid Mao ‘Ninja’ amesema mechi yao dhidi ya Simba ni ngumu sana na huwezi kutabiri nani atashinda katika pambano hilo ambalo linavuta hisia za wapenzi wa soka nchi.
Himid aliwaua Simba katika fainali ya Kombe la Mapindunzi January 13, 2017 kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango Danniel Agyei na Azam kutawazwa mabingwa mara tatu wa taji hilo.
Himidi amepiga story na shaffidauda.co.tz na kusema: “Nia yetu tunataka kushinda kwakuwa timu yetu ipo katika kiwango bora na hilo tutalidhibitisha, hivyo wajipange naomba mashabiki wajitokoze kuja kutuoa sapoti.”
“Kikosi chetu ni bora kwa kuwa kinawachezaji wanaojituma na kujitambua sisi kazi yetu ni kuhakikisha tunatoka na ushindi dhidi ya Simba wikiendi hii,” anasema Himid.
Azam inayoshikilia nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa imecheza mechi 19 na kujikusanyia alama 31 huku ikikabiliwa na mchezo mkali dhidi ya Simba wikiendi hii katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.