Ashangaa mtuhumiwa kuendelea kutamba mtaani
Amsaidia shilingi milioni MOJA mama aliyemwagiwa TINDIKALI Aagiza jeshi la polisi kuanza upya uchunguzi na mtuhumiwa kufikishwa mahakamani
Ahoji mwajiri kumtumikisha mtumishi miaka 9 bila likizo na bila mafao yeyote au michango hifadhi YA jamii
MKUU wa Mkoa wa Mbeya ameliagiza jeshi la polisi kuanza upya uchunguzi na kumfikisha mahakamani mtuhumiwa aliyemumwagia TINDIKALI Bi Fidea Lucas na kumsabishia ulemavu wa Jicho
Pia amewaagiza CMA kupokea malalamiko YA Fidea Lucas kufanya kazi miaka tisa bila likizo wala mafao yeyote
Hi Fidea Lucas amewasilisha malalamiko yake mbele YA Mkuu wa Mkoa wakati wa kusikiliza kero za wananchi katika Bujumbura wa a Mkapa utaratibu ambao Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ameuweka tangu ateuliwe
Kutokana na mahitaji YA matibabu Mkuu wa Mkoa amemchangia Bi Fidea shilingi milioni moja ili zimsaidie matibabu