Ivanovic achagua club yake mpya baada ya Chelsea.
Habari zinazidi kupamba moto kwa mchezaji Branislav Ivanovic kwamba muda wake wa kuendelea kuitumikia Chelsea umeisha na sasa hivi anatafuta maisha mengine nje ya club hiyo.
Everton imeonyesha kuhitaji huduma ya mchezaji huyo mwenye miaka 32 lakini vichwa vingi vya habari vinatoa taarifa kamba Ivanovic atajiunga club inayoshiriki ligi ya Mosow.
Gazeti maarufu la michezo nchini Russia Sports Express limeripoti Ivanovic atajiunga na club ya Zenit St Petersburg.
Ivanovic anategemewa kutangaza mkataba wa miaka miwili na nusu na club kubwa ya hiyo kutoka Russia. Ivanovic anategemewa kulipwa mshaharawa Euro milioni 5 kwa mwaka.
Katika maisha yake ya Chelsea Ivanovic ameshinda mataji mbali mbali yakiwemo Primier League mara mbili, FA Cup mara tatu, League Cup, Europa League na Championa League.