SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 14 Januari 2017

T media news

HII NDIO KILICHOMSHANGAZA LULU KWENYE VIDEO YA RAPA DARASSA

Msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael ambaye amekuwa msanii wa kwanza kufungua kipindi cha 'NgazKwaNgaz' mwaka 2017 ametaja video zake 20 ambazo zilimkosha sana na kumfurahisha mwaka jana.

Katika ngoma 20 zilizofunga vizuri mwaka kwa Lulu Michael wimbo wa Darassa 'Muziki' ndiyo umekamata nafasi ya kwanza.

Lulu anadai kwa mara ya kwanza alipoiona video hiyo kwanza alidhani huenda imefanywa nje ya Tanzania, na alihisi huenda imeongozwa na director kutoka nje na kudai hakufikiria kabisa kama imeongozwa na director kutoka nyumbani.

Hii ndiyo list kamili ya video ambazo zimemkosha sana Lulu Michael mwaka jana.  

01: Muziki ya Darassa (Tazama video hapo chini)

02: Company ya Justin Bieber

03: Koffi Anan ya Yemi Alade

04: Kajiandae ya Alikiba na Ommy Dimpozi                  

05: Kokoro ya Rich Mavoko Ft. Diamond Platnumz 

06: Sweet Mangi ya Nikki Wa Pili Ft. Chin Bees 

07: Do Good. ya Joe EL A.K.A Joel Amadi

08: Soldier ya Falz ft Simi

09: Nobody's Business ya Skales  Ft. Banky W

10: Mama ya Kiss Daniel

11: Bad” ya Tiwa Savage featuring starboy Wizkid

12: No Kissing Baby by Patoranking feat. Sarkodie.

13: Don't Mind ya Kent Jones

14: Ain't Your Mama ya Jennifer Lopez

15: Lover boy ya Barnaba Boy 

16: Perfect Combo ya Joh Makini feat Chidma

17: Moyo Mashine ya Ben Pol 

18: Dume suruali ya Mwana FA 

19: Kuliko jana by Sauti Sol 

20: Ado ado ya Moe Music