SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 12 Januari 2017

T media news

Hali Tete Kwa Waziri Prof Muhongo, Yabainika Alishiriki Vikao vya Kupandisha Bei ya Umeme

Siku chache baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo kusitisha kupandishwa kwa gharama mpya za umeme kwa madai kuwa hakushirikishwa katika mchakato huo, taarifa zimebainisha kuwa waziri huyo alishiriki katika kikao kilichoshauri uamuzi wa kulitaka shirika hilo liwasilishe mapendekezo ya bei mpya ya nishati hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la mwananchi toleo la Alhamisi, Januari 12, 2017 zilizeleza kuwa waziri alizuia kupandishwa kwa gharama za umeme kwa asilimia 8.5 kuanzia mwaka 2017  akisema kwa utaratibu TANESCO wanatakiwa ipeleke maombi ya bei EWURA maonbi ya bei mpya na kabla ya mamlaka hiyo kutangaza ni lazima waziri mwenye dhamana akabidhiwe ripoti ya mwisho.

Waziri Muhongo wakati akisitisha ongezeko hilo alisema kuwa alishtushwa na kutangazwa kwa bei mpya bila kupokea ripoti ya mwisho. Waziri alisema kuwa matatizo ya shirika hilo hayawezi kutatuliwa kwa kuwabebesha mzigo wananchi.

Licha ya waziri kueleza hayo yote lakini taarifa za uhakika zinaonyesha wazi kuwa alishiriki kikao cha wadau kujadili mpango kazi wa TANESCO Septemba 28 mwaka jana ambapo walikubaliana shirika hilo lipeleke maombi ya kuongeza bei EWURA kabla ya siku mbili yaani, Septemba 30. Kikao hicho  kilifanyika jijini Dar es Salaam kikiwashirikisha wadau kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Benki ya Dunia (WB) na TANESCO.

Siku mbili baada ya kikao hicho Waziri Muhongo aliandika barua kwenda kwa Waziri wa Fedha, Dkt Mpango akimueleza maazimio ya kikao hicho.

Waziri Muhongo alipoulizwa kuhusu barua hiyo na kufanya kikao hicho cha mpangokazi ambapo alisema kuwa kufanya kikao si jambo la kushangaza kwa kuwa amekuwa akifanya mikutano hiyo na wahisani mbalimbali kama Umoja wa Ulaya (EU), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Benki ya Dunia (WB).

Alipoulizwa kuhusu kushiriki vikao vya kupandishwa bei na kuandika barua kwa waziri wa fedha, Waziri Muhongo alisema kuwa nyaraka zote alizoandika hakuna sehemu pameonyesha kuongezwa bei ya umeme

Kwa upande mwingine EWURA imekiri mara kadhaa kuwa wamekuwa wakiishirikisha Wizara ya Nishati na Madini katika hatua mbalimbali za mchakato wa kupitia na hatimaye kutazanga bei ya umeme.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi alisema alishtushwa sana na kauli ya Waziri Muhongo kuwa hakushirikishwa kwenye upandaji wa bei ya umeme. Alisema mara kadhaa wamekuwa wakiandika barua kwenda wizara yenye dhamana kuhusu hatua za mchakato mzima.