SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 12 Januari 2017

T media news

Gondwe: Pandeni miti ili kukabiliana na ukame

Handeni. Wananchi wanaofanyabiashara ya kuchoma na kuuza mkaa katika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, wametakiwa kuhakikisha wanapanda miti kwenye maeneo yao ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kutokana na kuwepo tishio la ukame nchini.

Akizungumza na wananchi hao leo kwenye uzinduzi wa vituo maalum vya kuuzia mkaa vilivyoandaliwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS), Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe alisema kila mfanyabiashara anayechoma na kuuza mkaa lazima ahakikishe anapanda miti.

Alisema Serikali imeamua kuwaweka pamoja wafanyabiashara hao kwa kuwatengenezea vituo maalum vya kuuzia mkaa ambapo watakuwa na vibali vya shughuli hiyo huku Serikali ikiingiza kipato pia kwa wahusika kukata vibali.