SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 1 Desemba 2016

T media news

SERIKALI YA MAGUFULI NI KIBOKO,WAKATA MRIJA MWINGINE TENA

Naibu waziri wa ofisi ya Rais, Tamisemi, utumishi na utawala bora, Selemani Jafo, amepiga marufuku bodi za manunuzi kutoa zabuni kwa wakandarasi ambao hawana ofisi zinazowatambulisha katika maeneo yaoWaziri Jafo amepiga marufuku hayo mjini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya sheria mpya ya manunuzi kwa maafisa manunuzi mjini humo.

“Wakandarasi wengine wanapata tenda ya mabilioni ya fedha lakini hata ofisi maalum hawana, na bodi za manunuzi zimefanya na kumpitisha mtu ambaye hata ofisi ambayo inasema hii conduct person inapatikana sehemu fulani lakini watu hata ofisi hawana. Na wengine wana panga katika ofisi za ubabaishaji na hili ni jukumu letu sisi bodi ya manunuzi,” alisema Jafo.

“Watu wote watakaopatikana katika manunuzi ya serikali yetu waweze kuwa ni watu makini ambao mwisho wa siku tunapata ile kitu inayoitwa value of money. Ndugu zangu katika kupitisha sheria ya manunuzi mwaka huu matokeo yake ni kwamba kumelenga kuokoa fedha kubwa sana na fedha nyingi sana za wananchi,” aliongeza.

BY: EMMY MWAIPOPO