SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 1 Desemba 2016

T media news

MSANII DAYNA NYANGE AKATAA OFA ZA MA DIRECTOR WATATU LAIVU

Hitmaker wa wimbo wa ‘Komela’ Dayna Nyange amedai kuwa kuna watayarishaji watatu walitaka kuufanyia wimbo wa Komela video lakini aliwakatalia.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bngo cha EA Radio kuwa sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na baadhi ya vitu alivyovitaka havikukaa sawa.

“Nina directors zaidi ya watatu ambao wanataka kushoot video ya wimbo wa Komela lakini nilikataa kufanya nao kwa kuwa baadhi ya vitu vilikuwa havijakaa sawa,” amesema.

Dayna ameongeza kuwa video ya wimbo huo aliomshirikisha Bill Nas itatoka baada ya mwezi mmoja.