Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameliagiza jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Zavala kata ya Buyuni Ilala, Chiku Said baada ya kutuhumiwa kuuza viwanja vya watu pamoja na serikali kinyume na sheria.Polisi wakiwa wamemkamata mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Zavala kata ya Buyuni Ilala, Chiku Said kwa tuhuma za kuuza viwanja vya serikali kinyume na sheria.Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi kulalamika kwa kumtuhumu mwenyekiti huyo kuuza viwanja vya serikali kinyume na sheria bila kuwahusisha wajumbe wenzake hali ambayo imesababisha mgogoro mkubwa wa ardhi katika eneo hilo.
Hatua hiyo ilimfanya mkuu wa mkoa huyo kumtaka Afisa Ardhi wa Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela kuthibitishwa kuuzwa kwa eneo hilo kinyume na sheria.
“Mheshimiwa mkuu wa mkoa, ni kweli tulikuwa na eneo Block J lakini limeuzwa,” alisema afisa huyo “Nataka kuwaambia kitu mwenyeviti wa mtaa hawaruhusiwi kuuza eneo katika mtaa. Mimi ningewataka wenyekiti kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa ili kuepuka kutokea kwa hayo mambo,Baada ya kauli hizo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameliagiza jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.