SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 9 Novemba 2016

T media news

USHINDI WA TRUMP UMESABABISHA DOLA YA MAREKANI KUSHUKA NA KUYUMBISHA KWA SOKO LA HISA GHAFLA , SOMA KUJUA ZAIDI...


RAIS MTEULE WA MAREKANI  DONALD TRUMP

Na Sosy

Thamani ya dola ya Marekani pia imeshuka ghafla nchini marekani  kwa kinachodaiwa kuwa kulikuwa na mchuano mkali kati ya Donald Trump na Hillary Clinton ambapo matajiri wengi nchi marekani walitaji ushindi kuelekea kwa bi Clintony

Masoko ya hisa ya Asia yameyumba baada ya matokeo ya awali ya uchaguzi wa Marekani kuonyesha ushindi wa Donald Trump kuwa ya kuaminika.

Thamani ya dola ya Marekani pia imeshuka.

Viwango vya hisa katika Masoko yote makuu katika kanda hiyo ya Asia kwa sasa vimeshuka, huku pesa zikielekezwa katika hisa salama, dhahabu na sarafu ya Japan- yen.

Wakati huo huo sarafu ya Mexico -Peso imeporomoka kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa dhidi ya dola.

Kwa kiwango ambacho wafanyabiashara walitarajia ushindi wa moja kwa moja wa Hillary Clinton, hata mchuano mkali pekee unatosha kuyumbisha sarafu hiyo.

Wastani wa viwango vya hisa nchini Japan Nikkei 225 uko chini kwa 2.2% kuku lile la Hang Seng la mjini Hong Kong likishuka kwa 3.5% , hali kadhalika Shanghai pia limeshuka kwa 1.3%.